Description
Wasifu wa Mwandishi:
Maisha ya Fran Geiger Joslin yalisambaratika wakati mumewe alipofariki kutokana na maradhi ya saratani ya ubongo. Leo, anatoa tumaini kwa wanaoomboleza, hasa wajane. Fran anapenda kazi ya umisheni na pia kufundisha wanawake vijana. Kwa sasa, anatumika kama Rais wa Auntheticity Book House, shirika lisilo la kibiashara la huduma ya uchapishaji linalotoa mafundisho yaliyorahisishwa ya kichungaji katika vijitabu vidogo.
Muhtasari wa Kitabu:
SIO KWA AJILI TU YA WAJANE NA WAGANE…
Kitabu hiki cha Ujane kinadhihirisha na kuhalalisha uzito wa hisia za ndani wanazopitia wale wote wanaoomboleza kuondokewa na wenzi wao. Kama Raki wa kuaminika, kitabu hiki kitatembea nawe na kukuletea tumaini. Fran pia anatoa ujuzi kwa wachungaji, washauri, na maraki wa karibu wanaoleta faraja kwa waombolezaji wanapopitia mchakato huu wa kujaribu kuyaishi maisha katikati ya huzuni na furaha.

