Description
Wasifu wa Mwandishi:
Dk. Thomas Golding ni muhitimu wa chuo cha kitheologia kilichopo Dallas. Ametumika kama mkuu wa chuo cha huduma katika mji wa Adelaide, Australia kwa miaka 12. Amekuwa mchungaji katika makanisa kadhaa katika nchi ya Marekani na Australia. Kwa sasa, Dk. Golding huandika mafundisho ya kithiologia na kuyafundisha katika maeneo mbalimbali duniani. Yeye na mke wake Diana hutumia muda wao katika nchi za Marekani, Australia, na India. Hupendelea pia kupiga vyombo vya muziki, kupiga picha za mazingira ya asili, na kupika.
Muhtasari wa Kitabu:
Uanafunzi ni nini? Kanuni? Kitabu kingine cha ziada cha kusoma? Mwalimu wa kuigwa? Uanafunzi: Kumfuata Yesu ni kitabu kinachotupatia mwito wa kuwa wanafunzi wa Yesu na pia kuwasaidia wengine kuwa wanafunzi. Je utaukubali mwito huu?
