Description
Wasifu wa Mwandishi:
Dr. Thomas Golding ni muhitimu wa chuo kiitwacho Dallas Theological Seminary katika ngazi ya Shahada ya uzamili (ThM) na Shahada ya Uzamivu (PhD). Kwa miaka mingi amekuwa akifundisha na kushauri wanafunzi kama mkuu wa chuo kiitwacho College of Ministries nchini Australia. Kwa sasa, Dr. Golding ni mwandishi wa machapisho ya kitheolojia kwa ajili ya mafunzo na hufundisha pote ulimwenguni. Yeye na mkewe, Diane wanaishi Adelaide, Australia Kusini.
Muhtasari Kitabu:
Je, uko radhi kuikubali changamoto ya kuzitathmini tamaduni, mapokeo na jadi zako za kibinadamu dhidi ya uhalisia wa dunia iliyoumbwa na Mungu? Upinzani Baina ya Mungu na Utamaduni kinatupatia changamoto ya kufikiria na kupambanua baina ya kweli na uongo tuupatao kutoka katika tamaduni, kwa kuulinganisha na kweli kuu: Neno la Mungu
