Description
Wasifu wa Mwandishi:
Dr. Jeff VanGoethem ni muhitimu wa chuo cha Dallas Theological Seminary katika shahada ya umahiri na baadaye shahada ya uzamivu katika elimu ya Theolojia. Huduma take endelevu ya Miaka thelathini na mitano imejikita katika huduma ya kichungaji na kufundisha. Katika safari zake za mara kwa mara za kimisheni huko Afrika ya Mashariki huwafundisha na kuwaelekeza wachungaji. Kwa sasa, Dr. VanGoethem anamtumikia Mungu kama mchungaji kiongozi wa kanisa la Scofield Church la Dallas, Texas na mkufunzi wa masomo ya shahada ya umahiri katika chuo kikuu cha Dallas Theological Seminary. Yeye na mkewe, Karen, wanaishi katika eneo la Dallas.
Muhtasari wa Kitabu:
Je unalielewaje jukumu lako la uchungaji—au uongozi wa kanisa? Mungu Ana matarajio gani kwa wake aliowaita kulea na kuongoza wengine? Kuchunga Kanisa la Mungu ni Kitabu kinachofunua safari ya Immanuel, kijana ambaye anaingia kwenye uongozi wa kanisa baada ya mchungaji wa kanisa la kijijini kwao kufariki. Kitabu hike ni chachu kwa kila kiongozi kufuata namna Mungu anavyoongoza.
